Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati
ya Azam na Simba iliyochezwa jana (Machi 30 mwaka huu) Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam imeingiza sh. 26,455,000.
Watazamaji 4,741 walikata tiketi
kushuhudia pambano hilo ambapo Azam iliibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.
![]() |
SIMBA DHIDI YA AZAM |
Mgawanyo kwa mapato ulikuwa Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 4,035,508.47, gharama za kuchapa tiketi
sh. 3,908,686 wakati kila klabu ilipata sh. 5,460,687.63.
Uwanja sh. 2,776,620.83, gharama za
mechi sh. 1,665,972.50, Bodi ya Ligi sh. 1,665,972.50, Mfuko wa
Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 832,986.25 na Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 647,878.19.
by BONIFACE WAMBURA
ule uyanga na usimba sasa unaenda kukoma
ReplyDelete