![]() |
Real Madrid katika picha ya ubingwa |
Real Madrid wameweza kuibuka na ushindi wa
magoli mawili kwa kwa moja dhidi ya
mahasimu wao wakubwa Barcelona katika mchezo wa fainali wa kombe la Copa del
rey.
Real wao
ndio walikuwa wa kwanza kupachika goli kunako dk ya 11 kupitia kwa Angel Di
maria, na hivyo kufanya hadi kipindi cha
kwanza kinamalizika Real walitoka wakiwa kifua mbele katika awamu hiyo.
Kunako
kipindi cha pili katika dk ya 68 kinda
wa Barcelona Marco Bartra aliweza kusawazisha bao hilo kupitia
mpira wa kichwa baada ya kuitumia vizuri kona iliyo chongwa na nahoza wake
Xavi.
Baada ya
goli hilo Barcelona waliweza kuamka na kujaribu kuonyesha mpira ulio
takata kama ilivyo kawaida yao, lakini
kunako dakika za lala salama Gareth Bale aliweza kuifungia real goli la
ushindi.
Bale aliweza
kusibitisha kuwa yeye ni mchezaji ghali zaidi duniani baada ya kumshinda mbio
kinda Marco Bartra na kwenda kumuona golikipa Pito kunako dk ya 85 ya mchezo
huo.
![]() |
bale akishangilia goli la ushindi |
Mchezo huo
ambao ulitawaliwa na kadi 5 za njano pia ulikuwa ni mchezo usio isha tamwe za
hapa na pale baina ya wachezaji wa timu hizi mbili, huku real wakiwa wameshuka
dimbani bila ya Cristian Ronaldo baada ya kupata majeraha ya nyama za pacha
katika mechi iliyopita.
Hii inakuwa
ni kwa mara ya 19 kwa real madrid walio chini ya Carlo Ancelotti kuweza
kuchukuwa kombe hili la Copa Del Rey
tangu lianzishwe na mara ya mwisho walichukuwa mwa 2010-2011 na mara ya
kwanza ilikuwa ni 1905.
![]() |
hakuna kama mimi |
Hili
linakuwa ni kombe la kwnza kwa Real Madrid kuweza kuchukuwa katika msimu huu,
huku wakiwa bado katika kugombania ubingwa wa ligi dhidi ya vinara wa ligi hiyo
kwa sasa ambao ni Atiletico De Madrid wenye alma 82 kwa 79 za real.
Lakini pia
unakuwa ni ubingwa wa kwanza kwa Carlo Ancelotti akiwa na klabu hiyo huku bado
akiwa na kibarua kizito cha kuipatia Real ubingwa wa mara ya 10 wa klabu bingwa
barani ulaya baada ya kuingia hatua ya nusu fainali na watakipiga na Bayern
Munich ya Ujerumani tarehe 22 mwezi huu.
No comments:
Post a Comment