Michuano ya hatua ya robo fainali ya klabu bingwa barani
ulaya inaendelea hii leo kwa kuzikutanisha timu kubwa nne kutoka ligi kuu tatu
tofauti barani ulaya ambazo ni Ujerumani, Uingereza, Spain, huku tukishuhu timu
tatu kati ya timu nane zilizoingia kwenye hatua ya robo fainali zikitoka kati
la liga.

Mashetani wekundu ambao wamekuwa na matokeo mabaya kwa msimu
huu leo hii watawakaribisha mabigwa watetezi wa taji hilo na mabingwa wapya wa
ligi kuu ya Ujerumani Bayern Munich
katika dimba la Old Traford.
Kocha David Moyes anategemea kukutana na upinzani mkubwa
kutoka kwa mabingwa hao wa ujerumani kutokana na kikosi walichonacho msimu huu
ambacho kimeweka rekodi ya kuchukuwa ubingwa huku wakiwa na mechi saba mkononi
ikiwa ni chini ya Pep Guadiola.



No comments:
Post a Comment