Ezequiel Lavezzi alitangulia kuwapa PSG
Bao la kuongoza katika Dakika ya 4 baada kuweka gambani Mpira
uliookolewa kwa Kichwa na John Terry na kufumua Shuti moja kwa moja na
kumpita Kipa Petr Cech.
![]() |
lavezzi akishangilia goli |
Chelsea walisawazisha kwa Penati ya
Dakika ya 27 iliyopigwa na Eden Hazard na ilitolewa na Refa Milorad
Mazic kutoka Serbia alipoamua Sentahafu wa PSG Thiago Silva
‘kamwangusha’ Oscar.
Hadi Mapumziko Bao zilikuwa 1-1.
PSG walifunga Bao lao la 2 baada ya
Ezequiel Lavezzi kupiga mpira safi ambayo Kipa Petr Cech alishindwa
kuzuia na kumparaza Zlatan Ibrahimovic kisha Mchezaji wa Chelsea David
Luiz kuusindikiza wavuni.
![]() |
Ibra kadabra akiwa kwenye maumivu makali ya misuli |
Mchezaji alietoka Benchi, Javier
Pastore, aliipa PSG Bao la 3 katika Dakika ya 90 baada ya kupokea Mpira
wa kurushwa na kuwatoka Cesar Azpilicueta, Frank Lampard na John Terry
kisha kupiga Shuti la chini chini na kumshinda Kipa Petr Cech,
timu hizi zitarudiana huko Stamford Bridge Jumanne Aprili 8.
sikutegemea kama hawa PSG wanaweza ichalaza Chelsea
ReplyDelete