AZAM FC itamkosa mchezaji wake chipukizi anayeinukia vizuri, Bryson
Raphael katika mchezo wake wa kesho wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
Meneja wa Azam FC, Jemadari Said amesema mchezaji huyo amerejea kutoka
Kenya alipokwenda kuichezea timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa
miaka 20, Ngorongoro Heroes akiwa anachechemea kwa maumivu ya kifundo
cha mguu.
Jemadari amesema hilo ni pigo kwa timu kwa sababu huyo ni miongoni mwa
wachezaji muhimu, lakini kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog atalazimika
kumuondoa mchezaji huyo katika programu yake ya kesho.
Tayari Azam FC inawakosa Samih Haji Nuhu, Joseph Kimwaga, Ismail Gambo
‘Kussi Jr’, Farid Mussa na Ibrahim Mwaipopo ambao wote ni majeruhi kwa
muda mrefu sasa.

No comments:
Post a Comment