Gareth Bale ndie aliefunga Bao la Kwanza
katika Dakika ya 3 tu baada kuunganisha pasi safi ya Daniel Carvajal na
kumzidi akili Kipa Roman Weidenfeller
![]() |
bale akiwa kazini |
Bao la Pili la Real lilifungwa katika Dakika ya 27 kupitia Isco kwa Shuti la chini toka Mita 20.
Hadi Mapumziko ilikuwa Real 2 Dortmund 0.
Katika Dakika ya 57, Mchezaji Bora
Duniani, Cristiano Ronaldo, alipiga Bao la 3 baada kumtoka Kipa Roman
Weidenfeller kufuatia kupokea pasi safi ya Luka Modric.
Likiwa ni bao la 14 kwa Ronaldo kwenye
UEFA CHAMPIONS LEAGUE msimu huu na ameifikia Rekodi ya Lionel
Messi aliyefunga Bao 14 katika Mechi 11 za UEFA CHAMPIONS LEAGUE msimu wa
2011/12 wakati Ronaldo amechukua Mechi 8 tu.
![]() |
bale na ronaldo wakipongezana |
Lakini laweza kuwa pigo au laa maana Ronaldo hakumaliza Mechi hii baada ya kuumia na kutolewa nje katika Dakika ya 80 na hadi sasa bado haijajulikana kama atakuwa tayar akatika mechi ya marudiano huko
Signal Iduna Park, Jijini Dortmund, Germany Jumanne Aprili 8.
No comments:
Post a Comment