Wednesday, 16 April 2014

KLABU MOJA WAPO KATI YA HIZI NNE LAZIMA ITAANDIKA REKODI MPYA KAMA IKIWA BINGWA WA UEFA



Mambo ambayo yanaweza kutokea na kuwa historia mpya na ya kipekee katika soka hususani katika ligi ya mabingwa barani ulaya yani UEFA, kwa msimu huu ambao tumeweza kushuhudia vilabu mbalimbali vikitoa upinzani wwa kutosha kwa vilabu kongwe katika ligi hiyo.

Tukianza na klabu ya Atletico de Madrid akiongozwa na Diego Simione ameweza kutoa upinzani mkubwa sana msimu huu akianzia katika ligi kuu ya spain yani La Liga na hadi sasa inaongoza ligi hiyo kwa tofauti ya pointi nne dhidi ya Barcelona.

Atletico imeingia katika hatua ya nusu fainali kwa kuwasambaratisha vizuri tu vigogo wengine kutoka katika ligi moja nao ambao ni fc Barcelona kwa jumla ya magoli 2 kwa 1 na hivyo kupelekea wao kuweza kuingia katika hatua hiyo ya nusu fainali na kukutana na Chelsea.

Kama watafanikikupita  kupita katika hatua hii na kuingia fainali na kufanikiwa kuchukua kombe hili namba mbili kwa umarufu duniani basi watakuwa wameweka rekodi mpya katika klabu tangia kuanzishwa yapata miaka 40 sasa kuchukuwa kombe hilo la UEFA kwa mara ya kwanza, Hiyo itakuwa ni kwa upande wa wababe hawa wapya wa ligi ya spain.

Kwa upande wa mabingwa wapya na wa kihistoria wa Ujerumani Bayern wao wameweza kuingia kwenye hatua ya nusu fainali baada ya kuwachabanga vilivyo mashetani wekundu wa jiji la manchester kwa jumla ya magoli 4 kwa 2 na kukata tiketi hiyo na sasa watkutana na Real Madrid.

Klabu hii inayongozwa  na kocha aliyejizolea makombea mbalimbali akiwa na Fc Barcelona Pep Guadiola kama itaweza kuchukuwa kombe hili basi itakuwa ni timu ya kwanza katika historia ya michuano hii kubeba kombe hili mara mbili mfululizo kwani wao ndo mabingwa watetezi hadi hivi sasa.

Kwa upande wa klabu ya Chelsea inayonolewa  na kocha mreno mwenye maneno mengi kama wasemavyo mashabiki wa soka dunia kwa ujumla Jose Mourinho, kama itafanikiwa kuchukua kombe hili basi itakuwa ni historia mpya kwa kocha huyo kuchukuwa kombe hili mra tatu akiwa na timu tatu tofauti na katika nchi tatu tofauti duniani.

Nao Real Madrid ambayo imeweza kuchukuwa kombe hili kwa mara 9 na kuwa klabu inayo ongoza katika hisoria ya michuano hii, basi kama itaweza kubeba tena kombe hili itakuwa ndiyo klabu ya kwanza katika historia kuweza kufikia nambari 10 au ( double digit number )

Je ni nani ataweza kuibuka mshindi na kuweka historia mpya katika klabu yake kati yao?, hili ni swali ambalo nazani tunaweza kulijibu kunako usiku wa tarehe 22 mwezi huu kati nchi ya Spain ambapo ndipo mechi zote za hatua ya nusu fainali zitaanzia.




No comments:

Post a Comment