Leo majira ya saa nane mchana ilifanyika droo ya kupanga timu zitakazo pambana katika raundi ya nne bora katika mashindano Champions league,mechi za kwanza zitachezwa tarehe 22 April 2014,mechi zote mbili zitaanza kuchezwa katika ardhi ya Hispania
Real madrid vs Bayern munchen
Atletico madrid vs Chelsea
Chelsea wanataka kufanya vizuri ili waweze kuonyesha yale waliyoyafanya mwaka 2012 dhidi ya Bayern munchen
Bayern munchen nao wanataka kuwa timu ya kwanza kuchukua kombe mara mbili mfululizo hivyo wana kazi ngumu dhidi ya Real madrid inayoongozwa na Cristiano ronaldo ,benzema na bale hao ni baadhi tuu
Atletico madrid nao wanataka kuweka historia kwa kuingia fainali hivyo tutegemee mechi nzuri zenye ushindani wa kutosha.
Real madrid nao watataka wafanye vizuri na kuendelea kuwa timu yenye makombe mengi zaidi katika mashindano haya.
Kazi ipo katika mechi hizo kila timu ikitaka kufanya vizuri ili kuweza kufanya vizuri katika kuelekea fainali.
Mwandishi-Ally giningi Shambi


No comments:
Post a Comment