Mechi ya kiporo iliyochezwa jana usiku kati Tottenham na
sunderland iliweza kutosha kuirudisha Manchester united katika nfasi yake ya
saba ambayo imekuwa nafasi ya kudumu kwa klabu hiyo katika msimu huu ambao
umekuwa wa majanga kwao.
Shukurani za pekee ziende kwake Emannuel Adebayor kwa kuweza kupigilia misumari miwili
katika ushindi wa goli tano kwa moja katika mchezo uliopigwa kunako dimba la
white hart line, na sunderland wao ndiyo walikuwa wa kwanza kupata goli kunako
dk ya 17 kupitia kwa Cattermole.
Lakini baadaye Adebayor aliuwasha moto wa kifuu kunako dk ya
28 huku Kane akimpokea kijiti hiko kunako dk ya 59 kwa kufunga goli la pili
lakini Eriksen naye alipigilia msumari wa tatu katika dk 78 na baadaye tena Yule
Yule Adebayor alipeleka msiba wan ne kunako dk ya 86.
Kabla ya mpira kumalizika yani katika dakika za lala salama
yani dk 90 Sigurdsson aliweza kuihakikishia sunderland kuwa swala la wao kushuka
daraja lipo pale pale baada ya kupiga goli la tano katika mchezo huo.
![]() |
Kwa ushindi huo wa spurs ulitosha kuipeleka katika nafasi ya
sita ya msimamo wa ligi na kuishusha Manchester United hadi nafasi ya saba kwa
tofauti ya pointi mbili, lakini pia ushindi huo uliendelea kuibakiza sunderland
katika jinamizi la kushuka daraja wakiwa katika nafasi ya mwisho na pointi 25.
Kocha wa sunderland Gus Poyet amedai kuwa itahitajika maajabu wao kuweza
kusalia katika ushindani wa ligi kuu ya uingereza kwa msimu ujao baada ya kuwa
na matokeo mabaya na sasa wanashika nafasi 20 huku wakiwa wamecheza mechi 31
tofauti ya mechi mbili na Fulham na Cardiff walio nafasi ya 18, 19.
Kwa upande wa pili kocha wa Totternham Tim Sherwood
alikaririwa akisema kuwa ilikuwa ni mechi nzuri na alifurahishwa sana na
kiwango cha timu yake kwa jana japo kuwa kuna tetesi huenda akaachia ngazi
mwisho wa msimu huu na kibarua hiko kikamuangukia Louis Van Gaa.

No comments:
Post a Comment