Manchester
united jana walifikia mwisho wa safari yao ya kuelekea kwenye hatua ya nusu
fainali ya klabu bingwa barani ulaya baada ya kupokea kichapo cha goli tatu kwa
moja kutoka kwa mabingwa watetezi wa taji hilo Bayern Munich.
Magoli
katika mechi hiyo yalifungwa na Patrice Evra kwa upande wa Man Utd kunako dk ya
57 huku Mario Manduzuck akisawazisha kunako dk ya 59 dk mbili baada ya goli la
Patrice Evra, huku Muller akipigilia msumari wa pili katika dk ya 68 na Robben
kumaliza katika dk ya 76.
![]() |
Evra akiwa ofisin kwake |
Ulikuwa ni
usiku mzuri snana kwa Pep Guadiola baada ya kuweza kuvitoa vilabu viwili
vikubwa kutoka katika ligi ya uingereza na kufika hatua ya nusu fainali huku
wakiwa na ndoto za kulitetea taji lao kwa mara ya pili, Bayern ilianzia kwa
Arsenal kwa kuwatoa na imemalizia kwa mashetani hao wekundu wa jiji la
Manchester.
![]() |
Dante akiongoza jahazi la furaha baada ya ushindi |
Nao fc Barcelona
jana waliweza kuyaaga mashindano hayo ya Uefa kwa kukubali kichapo cha goli
moja kwa bila kutoka kwa vinara wa ligi ya Spain ama la liga yani Atletico De
Madrid kwa bao la mapema tu kutoka kwa Koke katika dk 5.
![]() |
Koke akishangilia goli lake |
Ilikuwa ni
safari nzuri kwa kocha Diego Simione kwa usiku wa jana kuweza kuvuka hatua hiyo
ya robo na kuingia nusu fainali kwa kuwasambaratisha vigogo hao kutoka La
massia , ilikuwa ni mechi ya kukata na shoka kwani wote wanatoka kwenye ligi
moja na huku wakiwa wamefuatana wakwanza na wa pili.
![]() |
tumemaliza kazi |
Kwa matokeo
ya jana na juzi yameweza kutoa timu nne ambazo zitamenyana kwenye hatua ya nusu
fainali ya michuano hiyo, Spain wao wamefanikiwa kutoa timu mbili kuelekea
hatua hiyo ya nusu fainali ambazo ni Real Madrid na Atiletico De Madrid.
Chelsea
ndiotimu pekee iliyoweza kuvuka kwa timu za uingereza baada ya kuwatoa Psg na
Bayern Munich imeweza kuiwakilisha Ujerumani katika hatua ya nusu fainali baada
ya ndugu Dortmund kushindwa kufuzu mbele ya Madrid.
Huenda
kukawa msisimko wa michuano hii kuelekea kwenye fainali ya michuano hii huko
Lisbon Ureno baada ya makocha wawili walio wahi kufundisha Chelsea na Madrid
kutabiriwa kukutana katika nusu fainali ambao ni Mourinho na Carlo Ancolotti.
No comments:
Post a Comment