Siku zote huwa nasema mpira ni mchezo wa dadika 90 na hilo
halina ubishi na kwa kusibitisha hilo usiku wa jana tuliweza kushuhudia vijana
wa Jose Mourinho wakiibuka na ushindi wa magoli 2 kwa bila dhidi ya Matajiri wa
Ufaransa yani Psg.
Magoli hayo mawili ndizo zilikuwa ndoto za special one tangu
alipo poteza mchezo wa kwanza kule Ufaransa kwa jumla ya magoli 3 kwa 1 akiwa
ugenini, na hivyo kumfanya awe jna kibarua kikubwa zaidi cha kubadili matokeo
jambo ambalo alifanikiwa hiyo jana akiwa katika uwanja wa nyumbani.
Goli lililoamsha matumaini ya kusonga mbele katika hatua ya
nusu fainali lilifungwa na Schurrle aliyeingia kuziba pengo la kijana mtundu wa
dimba la kati Edun Hazard kunako dk ya 32 na hivyo kuipeleka chelsea mapumziko
wakiwa na uhakika wa kusonga mbele.
Mabadiliko ya dakika za lala salama yaliweza kuzika kabisa
ndoto za Psg kufika hatua ya nusu fainali na ni pale alipotoka Lampard na
kuingia BA kunako dk 66, na ilipofika dakika ya 87 BA aliweza kumkamilishia
vizuri kabisa kocha wake safari ya kurudi Bernabeu kwa nusu fainali dhidi ya
real madird.
![]() |
Ba akifunga goli la ushindi |
Katika mchezo mwingine uliopigwa huko Ujerumani Real Madrid
waliweza kusonga mbele kwa mtaji mzuri wa magoli matatu bila walio shinda
nyumbani katika mechi ya kwanza dhidi ya
Dortimund japo ya kukubali kipigo cha goli 2 kwa bila hiyo jana.
Wenyeji wa mchezo huo walioshambulia kwa kasi zaidi katika
dakika takribani zote walijipatia goli kunako dk ya 24 kupitia kwa Marco Reus
baada ya Real kukosa penati katika dak ya 18 iliyopigwa na Di maria baada ya
kipa kuicheza penati hiyo.
Kunako dk ya 37 tena yule yule Marco Reus aliweka kambani na
kufanya mpira uwe wa kasi na ushindani zaidi kwa pande zote mbili huku madrid
wakijaribu pia kuliandama lango wa Dortmund mara kwa mara.
Jana Real walishuka dimbani bila ya Ronaldo baada ya kuumia
kwenye mechi ya kwanza na hivyo kulipelekea kwa walinzi wa Dortmund kupumzika
na kufanya kazi yao kwa kujiamini zaidi kwani safu ya Karimu Benzema na Bale na
Di maria haikuwa moto wa kutisha sana.
![]() |
Reus akishangila na wenzake |
No comments:
Post a Comment