Bayern Munich wametangazwa kuwa mabingwa wa ligi kuu ya
ujerumani maarufu kama Bungesliga hapo jana baada ya kuwafunga Hertha BSC magoli 3 kwa 1 na
kufikisha jumla ya pointi 77 na wakiwa wamecheza michezo 27, na hivyo hakuna
timu ya kufikia idadi hiyo ya pointi kwani bado wana michezo saba mkononi.
Borussia Dortmund ndiyo wanashika nafasi ya pili kwa sasa
wakiwa na pointi zao 57 na wakiwa wamecheza
michezo 27 sawa na Bayern lakini kukiwa na gepu kubwa la pointi ambalo
ni ngumu kulifikia kwa sasa.
Hii inakuwa ni rekodi mpya kwa club hiyo na kwa ligi hiyo
pia, lakini imekuwa ni rekodi nyingine kwa kocha wa klabu hiyo Pep Guardiol
kuweza kuchukua kombe la ligi huku akiwa na mechi saba mkononi.
Ukiwa ni msimu wake wa kwanza katika klabu ya Bayern tayari
ameshaweka kibindoni makombe matatu kati ya matano anayoshiriki na timu yake,
ambapo amefanikiwa kuchukuwa Club World Cup, Super Cup, Bundesliga, na sasa bado
wamefanikiwa kuingia katika robo fainali ya klabu bigwa ulaya na pia wapo
katika hatua ya nusu fainali ya German Cup.
Kwa mana hiyo kama mambo yatakwenda sawa huenda Pep guardiol akaweka rekodi mpya katika vitabu
vya ligi hiyo kwa kuwa kocha wa kwanza kuchukuwa makombe yote ambayo ameweza
kushiriki kwa msimu moja.
Baada ya
mechi ya jana kumalizika pep alisikika akisema kuwa ( Nashukuru tumemaliza
salama na tayari tunalo hili kombe mkononi mwetu, lakini napenda kuwashukuru
viongozi wa timu na wachezaji pia bila kusahau bechi langu la ufundi pia kwani
wao ndo kila kitu. )
Kwa sasakikosi hiko cha Bayern kimebaki na kazi moja ambayo ni
kuhakikisha wanashinda mechi zote saba zilizobaki ili kujiwekea rekodi ya
kipekee ya kumaliza ligi huku wakiwa na pointi tisini na moja ( 91 ).

No comments:
Post a Comment