Kocha wa vijana wa darajani ( Chelsea ) atangaza njaa kali kwa baadhi ya wachezaji wake na kudai kuwa huenda akafany6a mabadiliko makubwa sana baada ya kupoteza michezo mitatu dhidi ya West Brom, Stoke City, na Crystal Palace.
The
special one amedai kuwa baadhi ya wachezaji wameonyesha ubinafsi katika baadhi
ya mechi kitendo kilichopelekea Chelsea kupoteza pointi muhimu na kukubali
kushuka katika kiti cha kugombania taji la ligi hiyo ya wingereza huku wakibaki
na pointi (69).
![]() |
KOCHA WA CHELSEA JOSE MOURINHO |
Mourinho ameenda mbali na kusema bila kuficha kuwa katika
mechi ya juzi na Crystal Palace ambayo
walilala kwa bao moja kwa bila, baadhi ya washambuliaji wake walikosa nafasi za
wazi kabisa na hivyo kupelekea kupoteza pointi tatu muhimu.
Baada ya mechi hiyo
Mourinho alikaririwa akisema kuwa “ Hili liko wazi na hakuna asiyejua
kuwa msimu ujao Chelsea itakuwa na mshambuliaji mpya katika kikosi chake , na
kuhusu nini kitatokea kwa wengine basi lipo wazi kama mchezaji atakuwa hana
furaha na hajacheza mechi nyingi basi hapa si mahala pake”.
Hadi sasa Chelsea inayo washambuliaji watatu ambao ni Samwel
Etoo, Demba Ba, na Fernando Torres, ambao hivi sasa wameshukiwa na zigo la
lawama na huenda kukawa na sitofahamu juu ya uwepo wao kunako klabu hiyo ya
jiji la London.
Kwa upande huenda klabu ya Chelsea ikafanikiwa kumnyaka
mshambuliaji hatari kwa hivi sasa kunako ligi kuu ya spain Diego Costa
anayekipiga katika klabu ya Atletico Madrid, na hivyo kupelekea baadhi ya
majini kama Torres, David Luiz, Ashey Cole kutokuonekana msimu ujao kweny
kikosi hiko.
![]() |
DIEGO COSTA, KIBOKO YA MAGOLI ANEYEWINDWA NA CHELSEA |
Hata hivyo mourinho bado anakibarua kizito zaidi kwenye
michuano ya klabu bigwa ulaya ( UEFA )
dhidi ya matajiri wa ufaransa (PSG) watakapo kutana, na ameahidi kuwa mechi
iatkuwa ngumu lakini lazima wapigane kushinda na si vinginevyo.
No comments:
Post a Comment