Huenda dunia ikashanga haswa kwa wale mashabiki wa timu ya
taifa ya Brazil pale watakapo shuhudia timu ya taifa ya uingereza ikivaa jezi
sawa na zile za kwao katika moja ya mechi za kombe la dunia mwaka huu huko
Brazil.
Chama cha soka cha Uingereza FA kimetoa aina ya jezi amabazo
timu hiyo itatumia kwenye fainali hizo za kombe la dunia mwezi wa sita mwaka
huu, zikiwa na rangi nyeupe lakini pia za ugenini zikiwa na rangi nyekundu huku
zikiwa chini ya wadhamini wao wakubwa Nike.
![]() |
RANGI NYEUPE AMBALO NI CHAGUO LA KWANZA |
![]() |
RANGI NYEKUNDU AMBALO NI CHAGUO LA PILI |
Lakini habari za ndani ya FA zinasema kuwa kwa kushirikiana
na wadhamini wao Nike wanajiandaa kutoa jezi za rangi ya njano ambazo zitakuwa
sawa kabisa na zili za wandaaji wa fainali hizo za kombe la dunia yani Brazil.
![]() |
HII NDO JEZI AMBAYO ITAFANANA NA ZILE ZA BRAZIL |
Moja ya kiongozi wa FA alisikika akisema kuwa kama wanataka
kucheza kama Brazil basi lazima wajiandae kuwa kama Brazil kuanzia kimavazi ili
kufikia kiwango cha timu hiyo, lakini amebainisha kuwa huenda jezi hizo
zikatumika kwenye fainali kama watafanikiwa kufika hatua hiyo kubwa kabisa.
Kwa mujibu wa wa taarifa ya ndani kwenye chama hiko ni kuwa
jezi hizo ambazo zitatumiwa na timu hiyo huko Brazilb zitakuwa sokoni kuanzia
jumatatu, na mashabiki wa timu hiyo wanazisubiri kwa hamu sana kutokana na
jinsi zilivyo.
No comments:
Post a Comment