Tuesday, 8 April 2014

DONDOO KUELEKEA MECHI ZA MZUNGUKO WA PILI WA HATUA YA ROBO FAINALI YA UEFA



Habari njema kwa mashabiki wa klabu ya Manchester united ni kuwa huenda mshambuliaji wao tegemo kwa sasa katika kikosi hiko Wayne Rooney akacheza mchezo wa kesho baada ya kuwa nje ya uwanja  kutokana na kuumia  kidole gumba cha mguu wa kulia kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Bayern wiki iliyopita.

Rooney akiwa mazoezini
Kocha David Moyes amesibitisha kuwa mshambuliaji huyo ameshiriki katika mazoezi ya pamoja na wenzake kwa mda wote kabla ya kufunga safari ya kuelekea Ujerumani kuvaana na mabingwa watetezi wa kombe hilo la uefa hapo kesho kwenye dimba la Alias Arena.

Kwa upande wa Chelsea wao watafurahia kurejea kwa mpachika mabao wao aliyekuwa nje kwa kipindi cha wiki mbili Samuel Etoo baada ya kuumia misuli ya paja na kutoka nje kwenye pambano lao dhidi ya Arsenal huku akifunga goli la mapema katika ushindi wa goli 6 kwa bila walio upata.

Samwel Eto'o akiwa mazoezini
Etoo alikosekana kwenye mechi ya kwanza iliyopigwa huko Paris na kushuhudia Chelsea wakilala kwa goli 3 kwa moja dhidi ya wenyeji  PSG, na hivyo kupelekea kwa kocha mwenye maneno mengi Jose Mourinho kuwa na kibarua kizito leo kwenye dimba lake la nyumbani pale Darajani.

Hadi sasa Etoo ameweza kushuka dimbani myara 28 msimu huu na kuweza kufunga magoli 11 katika mechi zote lakini pia ameweza kutoa pasi zilizo zalisha magoli mara 3 huku akiwa na kadi 1 tu ya njano na hivyo kuwa na rekodi nzuri baada ya kupewa kipa umbele na kocha wake kama mshambuliaji namba 1.

Naye kocha wa Real Madrid amekanusha tetesi za kuwa huenda akamtumia winga wake wa gharama duniani Gareth Bale kuziba pengo la mbrazil Marcelo aliyeumia wiki moja iliyopita watakapo safari kwenye dimba la Iduna Park kukutana na Borrusia Dortmund kwa mchezo wa marudiano.

Gareth Bale
Taarifa hizo zilivuma kutokana na mchezaji huyo kuwa alianzia mpira akicheza kama beki wa kushoto akiwa katika klabu ya Southampton lakini hata alipo hamia spurs alikuwa akicheza namba hiyo kabla ya kubadilishwa na kuwa na winga wa kushoto mwenye uwezo wa kucheza kama mshambuliaji.



Bosi huyo wa wafalme hao wa  spain amedai kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kumchezesha beki wa kireno Fabio Contrao na kumbakiza Bale kunako nafasi yake ile ile  na hiyo itasaidia kuongeza zaidi mashambulizi pale mbele kwa Ronaldo na Karim Benzema.

No comments:

Post a Comment