Naweza kuita
kama huu ni mwaka wa mapinduzi katika ulimwengu huu wa kwetu wale wapenzia na
wafuatiliaji wazuri wa mpira wa miguu duniani kwa ujumla, kwa kusema kuwa kila kitu kinawezekana kama
kweli ukiwa na nia ya dhati katika jambo
husika.
Jana niliweza
kushuhudia Stevin Gerrad akijaribu kulia kwa hisia na kuonyesha kuwa ni jinsi
gani mpira ulivo sehemu muhimu katika maisha yake na ni baada ya kuwachapa Man
city magoli matatu kwa mawili na kuweza kujisogeza karibu kabisa na upepo wa
ubingwa wa ligi hiyo ya EPL.
Unajua ni
kwanini alilia na kushangilia kwa nguvu? Ni kwasababu bado hajapata nafasi ya
kulishika taji la ubingwa wa uingereza tangu aanze kuitumikia klabu hiyo ya
liverpool, na sasa anahisi ndo mda wake sahihi wa kuweza kulinyakuwa taji hilo
ambalo litakamilisha historia yake baada ya kuweza kunyakuwa mataji mbalimbali
ulaya.
Ukiachana na
hayo ya huko ulaya turudi hapa kwetu sasa ambapo kila siku tunasema soka letu
bado halijakuwa kutokana na mwenendo wa uendeshaji wa ligi yetu na jinsi tulivyo
tengeneza ama tunavyo viendesha vilabu vyetu.
Jana kwa
mara ya kwanza tuliweza kupata mgeni ama mbabe mpya katika soka la bongo kwa
kuchukuwa ubingwa wa ligi kuu bara na kufanikiwa kuvunja ule uyanga na usimba
uliyodumu kwa takiribani miaka kumi na nne sasa tangu pale mwaka 2000
alipochukuiwa Mtibwa sukari.
Azam Fc jana
waliweza kutangaza ubingwa kwa kuvunja historia ya watoto wa jiji la Mbeya yani
Mbeya city kunako uwanja wao wa nyumbani wa sokoine kwa kuwatandika goli mbili
kwa moja na kufikisha pointi 59 huku wakiwa na mchezo moja mkononi na hivyo
hakuna wa kufikia pointi hizo tena.
Yanga ambao
walikuwa wanapewa nafasi ya kunyakuwa taji hilo
wao waliweza kuchomoza na ushindi wa goli mbili kwa moja dhidi ya
wenyeji wa mchezo huo ambao ni Jkt Olijoro huko jijini Arusha na kufikisha
pointi 55 huku wakiwa na mechi moja mkononi dhidi ya Simba hapo Aprl 19.
![]() |
washafanya yao |
Ni baada ya
miaka saba sasa Azam Fc wameweza kukivuna kile ambacho walikipanda mnamo mwaka
wa 2008 kwa kupanda daraja na kushiriki rasmi katika ligi kuu ya Tanzania bara
maarufu kama ligi kuu ya vodacom.
Kuanzia
wachezaji, uongozi wa klabu , mazingira yanayoizunguka klabu kama viwanja vya
mazoezi uwanja wao wa nyumbani yani Chamanzi, basi utaweza kukubaliana na mimi
kuwa walistahili kuchuwa ubingwa msimu huu au hata iliyopita huko nyuma sema
mda ulikuwa bado haujafika nazani.
Nazani
tutakuwa tumejifunza kitu kwa sisi wale tulio na uyanga na usimba kuwa kuuza
wachezaji nje sio ndo kuendelea kwa mpira wetu bali inatupasa tuwekeze katika
mpira kulingana na mapato tunayoingiza kila siku.
Kuchukuwa
ubingwa kwa Azam naweza sema kuwa walikubali kuwekeza na walikubali kuvumilia
na walikubali kujifunza kutokana na makosa waliofanya misimu ya nyuma na sasa
wanaondoka katika jiji la mbeya wakiwa mabingwa wapya wa ligi kuu bara kwa mara
ya kwanza.
Kabla ya
Azam jana kubeba ubingwa na kuvunja usimba na uyanga vilabu hivi navyo viliweza
kuvunja mwiko huu kwa miaka tofauti tofauti, COSMO 1967, MSETO 1975, TUKUYU
STARS 1986, COASTAL UNION 1988, MTIBWA SUGAR 1999 NA 2000 NA sasa ni AZAM 2014.
Azam
wametupatia darasa la kutosha mashabiki na wadau wa soka hapa Tanzania kwa
ujumla kwani hakuna kinachoshindikana kama kweli ukiamua na nazani zikipatikana
timu kama Azam ziwe nne basi lazima soka letu linaweza kuifikia nchi kama ya
Kenya au Uganda.
Narudia kwa
kusema kuwa huu ni mwaka wa maajabu na mapinduzi katika soka na si hapa
tanzania tu bali duniani kwa ujumla, baada ya azam sasa nasubiria kuona rafiki
yangu Diego Simione akiweza kuchukuwa lile taji la La liga ama kombe la klabu
bingwa barani ulaya, hongera Azam kwa hili
No comments:
Post a Comment