Tuesday, 8 April 2014

TIMU ZIPI KUTANGULIA HATUA YA ROBO FAINALI LEO?




Hiyo ndio ratiba ya mechi ya siku ya leo,raundi ya 8 bora ikiwa ni mchezo wa pili baada ya mchezo wa raundi ya kwanza juma moja lililopita na matokeo kuwa:
REAL MADRID 3-0 B.DORTMUND
PSG 3-1 CHELSEA

Ni mechi ngumu zinazobeba hisia kubwa kutoka kwa mashabiki ,hivyo kusubiriwa kwa hamu,kwa upande wa B.Dortmund wanakazi kubwa ya kutafuta ushindi wa goli 4-0 ilikuweza kusonga mbele au 3-0 ili wacheze tena dk 30 za nyongeza, Dortmund watamtegemea zaidi mshambuliaji wao Lewandowski aliyekuwa na adhabu mchezo uliopita.


Real madrid nao wakiwa na washambuliaji hatari kwa sasa duniani ikiongozwa na Ronaldo,Benzema na Bale hawana cha kupoteza leo baada ya kuwa na mtaji mzuri wa goli 3-0 katika mchezo wao kwa kwanza dhidi ya Dortmund.

Mechi ya pili leo ya Chelsea vs PSG mechi hii ni nzuri na sio ya kukosa kabisa,Chelsea wako nyumbani leo wakitafuta matokeo mazuri ili waweze kusonga mbele katika mashindano haya.

Mourinho anasema kuwa kikosi chake kipo vizuri na wataingia uwanjani wakiwa na bashasha wakiiamini wanaingia uwanjani kwenda kubadilisha matokeo ya 3-1 waliyofungwa katika mchezo wao wa kwanza.

Tusubirie dakika 90 ndio zitakazo tuamulia nani mbabe .

No comments:

Post a Comment