Manchester
United yalazimishwa sare ya moja kwa moja katika uwanja wake wa nyumbani
maarufu kama MACHINJIONI na mabingwa wapya wa ligi kuu ya ujerumani yani Bayern
Munich huku kiungo wa kutumainiwa Bastan Schweinsteiger akisawazisha lakini na
kupewa kati nyekundu.
![]() |
TUMESAWAZISHA |
Nemanja
Vidic ndiye aliye ifungia United goli la kuongoza katika dakika ya 58 kupitia mpira wa kona
uliopingwa na Wayne Rooney huku Schweinsteiger akisawazisha katika dakika ya 68
baada ya kuunganisha mpira uliopigwa na
Mario Manzukich.
![]() |
NEMANJA AKIFUNGA GOLI LA KUONGOZA |
Katika mechi nyingine pia Barcelona ililazimishwa
sare ya moja kwa moja pia na vinara wa la liga yani Atletico de Madrid katika
uwanja wake wa nyumbamni yani Caump new, shukurani za zati ziende kwa Neymar do
Santos kwa goli lake la kusawazisha baada ya kuwa nyuma kwa goli moja
lililofungwa na Diego Sultan aliye ingia kuchukuwa nafasi ya Diego Costa baada
ya kuumia.
![]() |
DIEGO SULTAN NA WENZAKE WAKISHANGILIA GOLI |
Diego Costa
alitoliwa nje kunako dakika ya 27 tu ya mchezo huo baada ya kubanwa na nyama za
paja na hivyo kumpatia nafasi yake Diego Sultan, amabye aliipatia timu yake
goli la kuongoza katika kipindi cha pili cha mchezo huo .
![]() |
NEYMAR AKISHANGILIA |
Katika
mchezo wa United Bastan Schweinsteiger alipewa kati nyekundu baada ya kumchezea
rafu Wayne Rooney katika dakika za majeruhi na hivyo ataukosa mchezo wa
marudiano kunako dimba la Areas Arena huko Ujerumani.
![]() |
BAADA YA KADI NYEKUNDU |
No comments:
Post a Comment