Tuesday, 22 April 2014

BREAKING NEWS; DAVID MOYES AFUKUZWA RASMI MAN UTD

Kwa taarifa zilizotoka hivi punde ni kuwa aliyekuwa kocha Man Utd amefukuzwa rasmi kunako klabu hiyo
Moyes aliyudumu kwa miezi kumi katika kiti hiko cha ukocha katika klabu hiyo amefukuzwa baada ya kuwa na mfululizo wa matokeo duni akiwa kama mwalimu wa klabu hiyo.
David Moyes

Moyes ameweza kupoteza mechi sita katika uwanja wa nyumbani msimu huu, huku akiipeleka klabu hiyo nje ya michuano ya klabu bigwa barani ulaya yani UEFA ambapo kwa mara ya mwisho Utd kutoshiriki ilikuwa mwaka 1995.


Monday, 21 April 2014

BREAKING NEWS- MOYES KUONDOKA OLD TRAFFORD






Kwa habari zilizozagaa kwenye mitandao muda huu,kuna habari inayoelezea kuwa kocha wa Man utd David Moyes huenda akaondoka Old trafford

Bodi ya timu ya manchester wameshindwa kuvumilia suala hili baada ya kipigo cha jana cha 2-0 dhidi ya timu Everton.

Magazeti  kama Daily telegraph,daily mail na the guardian yote yameripoti kuhusu habari hii leo hii hivyo huenda Moyes asiweze kumalizia mechi nne zilizobakia.

klabu ya Manchester united mpaka sasa imeshindwa kukanusha juu ya habari hii,na viongozi walipoulizwa walijibu suala la kumfukuza Moyes ni suala suala linaloweza kutolea muda mchache ujao.

mwandishi-ALLY GININGI SHAMBI

Wednesday, 16 April 2014

EVERTON YAPUNGUZWA KASI, HUKU MAN CTY YALAZIMISHWA SARE YA KIPORO CHAKE DHIDI YA SUNDERLAND

mashabiki wa everton waliungana na wenzao wa liverpool kuwakumbuka mashabiki waliopoteza maisha katika  FC Hillsborough disaster kabla ya mchezo.
 Klabu ya Everton leo imepunguzwa kasi ya kuweza kuwania nafasi ya nne kwajili ya kushiriki ligi ya mabigwa barani ulaya UEFA baada ya kupokea kichapo kutoka kwa Crystal Palace na hivyo kurudi nafas ya 5.

 Nao Man cty wamelazimishwa sare na sunderland walio kweny nafasi ya mwisho ya msimamo wa ligi, baada ya kucheza mechi amabayo ilikuwa ni kiporo kwa timu zote mbili, na sasa Man cty anabaki na alama 71 huku bado akiwa na mchezo mkononi.

wickham akifunga goli la kwanza

KLABU MOJA WAPO KATI YA HIZI NNE LAZIMA ITAANDIKA REKODI MPYA KAMA IKIWA BINGWA WA UEFA



Mambo ambayo yanaweza kutokea na kuwa historia mpya na ya kipekee katika soka hususani katika ligi ya mabingwa barani ulaya yani UEFA, kwa msimu huu ambao tumeweza kushuhudia vilabu mbalimbali vikitoa upinzani wwa kutosha kwa vilabu kongwe katika ligi hiyo.

Tukianza na klabu ya Atletico de Madrid akiongozwa na Diego Simione ameweza kutoa upinzani mkubwa sana msimu huu akianzia katika ligi kuu ya spain yani La Liga na hadi sasa inaongoza ligi hiyo kwa tofauti ya pointi nne dhidi ya Barcelona.

Atletico imeingia katika hatua ya nusu fainali kwa kuwasambaratisha vizuri tu vigogo wengine kutoka katika ligi moja nao ambao ni fc Barcelona kwa jumla ya magoli 2 kwa 1 na hivyo kupelekea wao kuweza kuingia katika hatua hiyo ya nusu fainali na kukutana na Chelsea.

Kama watafanikikupita  kupita katika hatua hii na kuingia fainali na kufanikiwa kuchukua kombe hili namba mbili kwa umarufu duniani basi watakuwa wameweka rekodi mpya katika klabu tangia kuanzishwa yapata miaka 40 sasa kuchukuwa kombe hilo la UEFA kwa mara ya kwanza, Hiyo itakuwa ni kwa upande wa wababe hawa wapya wa ligi ya spain.

Kwa upande wa mabingwa wapya na wa kihistoria wa Ujerumani Bayern wao wameweza kuingia kwenye hatua ya nusu fainali baada ya kuwachabanga vilivyo mashetani wekundu wa jiji la manchester kwa jumla ya magoli 4 kwa 2 na kukata tiketi hiyo na sasa watkutana na Real Madrid.

Klabu hii inayongozwa  na kocha aliyejizolea makombea mbalimbali akiwa na Fc Barcelona Pep Guadiola kama itaweza kuchukuwa kombe hili basi itakuwa ni timu ya kwanza katika historia ya michuano hii kubeba kombe hili mara mbili mfululizo kwani wao ndo mabingwa watetezi hadi hivi sasa.

Kwa upande wa klabu ya Chelsea inayonolewa  na kocha mreno mwenye maneno mengi kama wasemavyo mashabiki wa soka dunia kwa ujumla Jose Mourinho, kama itafanikiwa kuchukua kombe hili basi itakuwa ni historia mpya kwa kocha huyo kuchukuwa kombe hili mra tatu akiwa na timu tatu tofauti na katika nchi tatu tofauti duniani.

Nao Real Madrid ambayo imeweza kuchukuwa kombe hili kwa mara 9 na kuwa klabu inayo ongoza katika hisoria ya michuano hii, basi kama itaweza kubeba tena kombe hili itakuwa ndiyo klabu ya kwanza katika historia kuweza kufikia nambari 10 au ( double digit number )

Je ni nani ataweza kuibuka mshindi na kuweka historia mpya katika klabu yake kati yao?, hili ni swali ambalo nazani tunaweza kulijibu kunako usiku wa tarehe 22 mwezi huu kati nchi ya Spain ambapo ndipo mechi zote za hatua ya nusu fainali zitaanzia.




GARETH BALE ASIBITISHA KUWA YEYE NIA HATARI BAADA YA KUIPATIA REAL UBINGWA WA 19 WA COPA DEL REY



Real Madrid katika picha ya ubingwa


Real  Madrid wameweza kuibuka na ushindi wa magoli  mawili kwa kwa moja dhidi ya mahasimu wao wakubwa Barcelona katika mchezo wa fainali wa kombe la Copa del rey.

Real wao ndio walikuwa wa kwanza kupachika goli kunako dk ya 11 kupitia kwa Angel Di maria,  na hivyo kufanya hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Real walitoka wakiwa kifua mbele katika awamu hiyo.

Kunako kipindi cha pili  katika dk ya 68 kinda wa Barcelona  Marco  Bartra aliweza kusawazisha bao hilo kupitia mpira wa kichwa baada ya kuitumia vizuri kona iliyo chongwa na nahoza wake Xavi.

Baada ya goli hilo Barcelona waliweza kuamka na kujaribu kuonyesha mpira ulio takata  kama ilivyo kawaida yao, lakini kunako dakika za lala salama Gareth Bale aliweza kuifungia real goli la ushindi.
di maria akishanglia goli la kwanza

Bale aliweza kusibitisha kuwa yeye ni mchezaji ghali zaidi duniani baada ya kumshinda mbio kinda Marco Bartra na kwenda kumuona golikipa Pito kunako dk ya 85 ya mchezo huo.

bale akishangilia goli la ushindi
Mchezo huo ambao ulitawaliwa na kadi 5 za njano pia ulikuwa ni mchezo usio isha tamwe za hapa na pale baina ya wachezaji wa timu hizi mbili, huku real wakiwa wameshuka dimbani bila ya Cristian Ronaldo baada ya kupata majeraha ya nyama za pacha katika mechi iliyopita.

Hii inakuwa ni kwa mara ya 19 kwa real madrid walio chini ya Carlo Ancelotti kuweza kuchukuwa kombe hili la Copa Del Rey  tangu lianzishwe na mara ya mwisho walichukuwa mwa 2010-2011 na mara ya kwanza ilikuwa ni 1905.

hakuna kama mimi
Hili linakuwa ni kombe la kwnza kwa Real Madrid kuweza kuchukuwa katika msimu huu, huku wakiwa bado katika kugombania ubingwa wa ligi dhidi ya vinara wa ligi hiyo kwa sasa ambao ni Atiletico De Madrid wenye alma 82 kwa 79 za real.

Lakini pia unakuwa ni ubingwa wa kwanza kwa Carlo Ancelotti akiwa na klabu hiyo huku bado akiwa na kibarua kizito cha kuipatia Real ubingwa wa mara ya 10 wa klabu bingwa barani ulaya baada ya kuingia hatua ya nusu fainali na watakipiga na Bayern Munich ya Ujerumani tarehe 22 mwezi huu.

Monday, 14 April 2014

HUU NDO MWISHO WA ZAMA ZA USIMBA NA UYANGA, KARIBU AZAM WANA WA LAMBA LAMBA



Naweza kuita kama huu ni mwaka wa mapinduzi katika ulimwengu huu wa kwetu wale wapenzia na wafuatiliaji wazuri wa mpira wa miguu duniani kwa ujumla,  kwa kusema kuwa kila kitu kinawezekana kama kweli ukiwa na nia ya  dhati katika jambo husika.

Jana niliweza kushuhudia Stevin Gerrad akijaribu kulia kwa hisia na kuonyesha kuwa ni jinsi gani mpira ulivo sehemu muhimu katika maisha yake na ni baada ya kuwachapa Man city magoli matatu kwa mawili na kuweza kujisogeza karibu kabisa na upepo wa ubingwa wa ligi hiyo ya EPL.

Unajua ni kwanini alilia na kushangilia kwa nguvu? Ni kwasababu bado hajapata nafasi ya kulishika taji la ubingwa wa uingereza tangu aanze kuitumikia klabu hiyo ya liverpool, na sasa anahisi ndo mda wake sahihi wa kuweza kulinyakuwa taji hilo ambalo litakamilisha historia yake baada ya kuweza kunyakuwa mataji mbalimbali ulaya.

Ukiachana na hayo ya huko ulaya turudi hapa kwetu sasa ambapo kila siku tunasema soka letu bado halijakuwa kutokana na mwenendo wa uendeshaji wa ligi yetu na jinsi tulivyo tengeneza ama tunavyo viendesha vilabu vyetu.

Jana kwa mara ya kwanza tuliweza kupata mgeni ama mbabe mpya katika soka la bongo kwa kuchukuwa ubingwa wa ligi kuu bara na kufanikiwa kuvunja ule uyanga na usimba uliyodumu kwa takiribani miaka kumi na nne sasa tangu pale mwaka 2000 alipochukuiwa Mtibwa sukari.

Azam Fc jana waliweza kutangaza ubingwa kwa kuvunja historia ya watoto wa jiji la Mbeya yani Mbeya city kunako uwanja wao wa nyumbani wa sokoine kwa kuwatandika goli mbili kwa moja na kufikisha pointi 59 huku wakiwa na mchezo moja mkononi na hivyo hakuna wa kufikia pointi hizo tena.

Yanga ambao walikuwa wanapewa nafasi ya kunyakuwa taji hilo  wao waliweza kuchomoza na ushindi wa goli mbili kwa moja dhidi ya wenyeji wa mchezo huo ambao ni Jkt Olijoro huko jijini Arusha na kufikisha pointi 55 huku wakiwa na mechi moja mkononi dhidi ya Simba hapo Aprl 19.

washafanya yao
Ni baada ya miaka saba sasa Azam Fc wameweza kukivuna kile ambacho walikipanda mnamo mwaka wa 2008 kwa kupanda daraja na kushiriki rasmi katika ligi kuu ya Tanzania bara maarufu kama ligi kuu ya vodacom.

Kuanzia wachezaji, uongozi wa klabu , mazingira yanayoizunguka klabu kama viwanja vya mazoezi uwanja wao wa nyumbani yani Chamanzi, basi utaweza kukubaliana na mimi kuwa walistahili kuchuwa ubingwa msimu huu au hata iliyopita huko nyuma sema mda ulikuwa bado haujafika nazani.

Nazani tutakuwa tumejifunza kitu kwa sisi wale tulio na uyanga na usimba kuwa kuuza wachezaji nje sio ndo kuendelea kwa mpira wetu bali inatupasa tuwekeze katika mpira kulingana na mapato tunayoingiza kila siku.
Kuchukuwa ubingwa kwa Azam naweza sema kuwa walikubali kuwekeza na walikubali kuvumilia na walikubali kujifunza kutokana na makosa waliofanya misimu ya nyuma na sasa wanaondoka katika jiji la mbeya wakiwa mabingwa wapya wa ligi kuu bara kwa mara ya kwanza.

Kabla ya Azam jana kubeba ubingwa na kuvunja usimba na uyanga vilabu hivi navyo viliweza kuvunja mwiko huu kwa miaka tofauti tofauti, COSMO 1967, MSETO 1975, TUKUYU STARS 1986, COASTAL UNION 1988, MTIBWA SUGAR 1999 NA 2000 NA sasa ni AZAM 2014.

Azam wametupatia darasa la kutosha mashabiki na wadau wa soka hapa Tanzania kwa ujumla kwani hakuna kinachoshindikana kama kweli ukiamua na nazani zikipatikana timu kama Azam ziwe nne basi lazima soka letu linaweza kuifikia nchi kama ya Kenya au Uganda.

Narudia kwa kusema kuwa huu ni mwaka wa maajabu na mapinduzi katika soka na si hapa tanzania tu bali duniani kwa ujumla, baada ya azam sasa nasubiria kuona rafiki yangu Diego Simione akiweza kuchukuwa lile taji la La liga ama kombe la klabu bingwa barani ulaya, hongera Azam kwa hili

Sunday, 13 April 2014

WAKENYA WATAMBA LONDON MARTHON


Mshikilizi wa rekodi ya dunia katika mbio za Marthon Wilson Kipsang alitwaa taji la mwaka huu la mbio za London Marathon alipoandikisha muda bora wa saa mbili dakika nne nukta 27 (2:04:27) .
Mkenya mwenza Stanley Biwott alimaliza katika nafasi ya pili akitumia muda wa saa mbili dakika nne nukta 55 ( 2:04:55)
Bingwa mtetezi wa mbio hizo Tsegaye Kebede kutoka Ethiopia alimaliza katika nafasi ya tatu akiwa ametumia muda wa saa mbili dakika sita nukta 30 (2:06:30).

Bingwa wa London marathon Wilson Kipsang
Katika kitengo cha wanawake wakenya walidhibitisha udedea wao walipotwaa nafasi za kwanza mbili .
Bingwa wa dunia Edna Kiplagat ambaye amemaliza katika nafasi ya pili katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita aljifurukuta katika kilomita ya mwisho na kumpiku Florence Kiplagat vilevile kutoka Kenya.

 .
Edna aliukata utepe baada ya kutimuka mbio hizo za kilomita 42 katika barabara za mji wa London akitumia muda wa saa mbili dakika 20 na sekunde 19 (2:20:19).

Bingwa wa dunia wa mbio mbio za kilomita 21 Florence Kiplagat,alimfuata kwa karibu sana akimaliza sekunde tatu tu nyuma yake .

Kiplagat alisajili muda wa saa mbili dakika 20 nukta 22 ( 2:20:22).
Methiopia mshindi wa dunia wa mbio za mita 5000 na mita 10,000 , Tirunesh Dibaba ambaye alikuwa akishiriki katika marathon yake ya kwanza alikamilisha mbio hizo katika nafasi ya tatu
Dibaba alisajili muda wa saa mbili dakika 20 na sekunde 33 ( 2:20:33).

Bingwa wa London marathon Edna Kiplagat

Edna ambaye aliweka jina lake katika vitabu vya historia kwa kuwa mwanamke wa kwanza kuwahi kushinda taji la marathon la dunia katika kipindi cha miaka miwili mfululizo aliiambia BBC kuwa alikuwa amechoshwa na nafasi ya pili.

''Mwaka wa 2012 nilimaliza wapili nyuma ya Mary Keitany akisajili muda wa 2:19:50
Mwaka wa 2013 nikashindwa hata baada ya kukimbia nikitumia muda wa (2:21:32) na Rita Jeptoo ,mwaka huu ilikuwa ni zamu yangu kuhakikisha nimeshinda''.

Ilikuwa shangwe na vigelegele kwa washindi wa mbio hizo walipolakiwa na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta aliyekuwa London kumpa mkewe motisha katika mbio hizo.

Bi Magret Kenyatta alishiriki mbio hizo katika azimio la kuchangisha fedha za kuimarisha huduma za afya kwa kinamama wajawazito katika maeno ya mashambani nchini kenya, anakusudia kutoa magari ya huduma ya kwanza katika majimbo yote 47 ya Kenya.

Bi Kenyatta alimaliza mbio hizo baada ya zaidi ya saa saba na kuwa mke wa rais wa kwanza duniani kuwahi kushiriki na kukamilisha mbio za marathon zenye umbali wa kilomita 42 .

Friday, 11 April 2014

TIMU HIZI KUKUTANA KATIKA RAUNDI YA NNE BORA ULAYA




Leo majira ya saa nane mchana ilifanyika droo ya kupanga timu zitakazo pambana katika raundi ya nne bora katika mashindano  Champions league,mechi za kwanza zitachezwa tarehe 22 April 2014,mechi zote mbili zitaanza kuchezwa katika ardhi ya Hispania

Real madrid vs Bayern munchen
Atletico madrid vs Chelsea

Chelsea wanataka kufanya vizuri ili waweze kuonyesha yale waliyoyafanya mwaka 2012 dhidi ya Bayern munchen

Bayern munchen nao wanataka kuwa timu ya kwanza kuchukua kombe mara mbili mfululizo hivyo wana kazi ngumu dhidi ya Real madrid inayoongozwa na Cristiano ronaldo ,benzema na bale hao ni baadhi tuu

Atletico madrid nao wanataka kuweka historia kwa kuingia fainali hivyo tutegemee mechi nzuri zenye ushindani wa kutosha.

Real madrid nao watataka wafanye vizuri na kuendelea kuwa timu yenye makombe mengi zaidi katika mashindano haya.
Kazi ipo katika mechi hizo kila timu ikitaka kufanya vizuri ili kuweza kufanya vizuri katika kuelekea fainali.

Mwandishi-Ally giningi Shambi

Thursday, 10 April 2014

MAN UTD, BARCELONA WAANGA UEFA, BAYERN ATLETICO DE MADRID WAINGIA NUSU FAINALI UEFA



Manchester united jana walifikia mwisho wa safari yao ya kuelekea kwenye hatua ya nusu fainali ya klabu bingwa barani ulaya baada ya kupokea kichapo cha goli tatu kwa moja kutoka kwa mabingwa watetezi wa taji hilo Bayern Munich.

Magoli katika mechi hiyo yalifungwa na Patrice Evra kwa upande wa Man Utd kunako dk ya 57 huku Mario Manduzuck akisawazisha kunako dk ya 59 dk mbili baada ya goli la Patrice Evra, huku Muller akipigilia msumari wa pili katika dk ya 68 na Robben kumaliza katika dk ya 76.

Evra akiwa ofisin kwake
Ulikuwa ni usiku mzuri snana kwa Pep Guadiola baada ya kuweza kuvitoa vilabu viwili vikubwa kutoka katika ligi ya uingereza na kufika hatua ya nusu fainali huku wakiwa na ndoto za kulitetea taji lao kwa mara ya pili, Bayern ilianzia kwa Arsenal kwa kuwatoa na imemalizia kwa mashetani hao wekundu wa jiji la Manchester.

Dante akiongoza jahazi la furaha baada ya ushindi
Nao fc Barcelona jana waliweza kuyaaga mashindano hayo ya Uefa kwa kukubali kichapo cha goli moja kwa bila kutoka kwa vinara wa ligi ya Spain ama la liga yani Atletico De Madrid kwa bao la mapema tu kutoka kwa Koke katika dk 5.

Koke akishangilia goli lake
Ilikuwa ni safari nzuri kwa kocha Diego Simione kwa usiku wa jana kuweza kuvuka hatua hiyo ya robo na kuingia nusu fainali kwa kuwasambaratisha vigogo hao kutoka La massia , ilikuwa ni mechi ya kukata na shoka kwani wote wanatoka kwenye ligi moja na huku wakiwa wamefuatana wakwanza na wa pili.

tumemaliza kazi
Kwa matokeo ya jana na juzi yameweza kutoa timu nne ambazo zitamenyana kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo, Spain wao wamefanikiwa kutoa timu mbili kuelekea hatua hiyo ya nusu fainali ambazo ni Real Madrid na Atiletico De Madrid.

Chelsea ndiotimu pekee iliyoweza kuvuka kwa timu za uingereza baada ya kuwatoa Psg na Bayern Munich imeweza kuiwakilisha Ujerumani katika hatua ya nusu fainali baada ya ndugu Dortmund kushindwa kufuzu mbele ya Madrid.


Huenda kukawa msisimko wa michuano hii kuelekea kwenye fainali ya michuano hii huko Lisbon Ureno baada ya makocha wawili walio wahi kufundisha Chelsea na Madrid kutabiriwa kukutana katika nusu fainali ambao ni Mourinho na Carlo Ancolotti.