Saturday, 29 March 2014

BADO MAPEMA KUMJUA BINGWA NANI KWA SASA KATIKA LIGI YA EPL


Hakika hapa ndipo unapotumika ile kauli ya kusema kuwa asiye fanya kazi na asile, ama kila mbuzi atakula kwa urefu wa kamba yake,  hii nia baadhi ya misemo ambayo hupendwa kutumiwa na wengi pindi panapokuwa na ushindani mkubwa wa kitu flani.
Nimeamua kutumia kauli hizi mbili au misemo hii miwili ambayo ina mana moja nazani katika matumizi ya kila siku.

Huku Pep Guadiola akikamilisha mapema tu kazi ya maafisa wa ligi kuu  ya ujerumani na kuwapa nafasi ya kupanga ratiba ya msimu ujao baada ya kuchukuwa ndoo ya ubingwa mapema tena akiwa na mechi saba mkononi na pia akiweka rekodi ya kipekee zaidi na kikosi cha bayern munich.

Lakini mambo yamekuwa tofauti sana kwa baadhi ya ligi kuu barani ulaya, hususani  kwa ligi kuu ya wingereza maarufu kama ( EPL ), kwani hadi kufikia sasa bado hajajulikana na atakaye tangazwa bigwa  mwishoni mwa msimu huu kati y Chelsea, Man cty, Liverpool, ama Arsenal.

Timu hizi zote bado zina nafasi ya kuchukuwa taji la ligi kama kila mmoja atatumia vizuri makosa atakayo yafanya mwenzake kwa wakati huu uliobakia kwenda kukamilisha mzunguko wa ligi hiyo, lakini ugumu unakuja kutokana na matokeo ambayo yamekuwa yakifanya ligi hii ya  EPL  kutumia ile misemo niliyo anzanayo mwanzo kabisa.

Baadhi ya matokeo ya leo katika ligi hiyo naweza seama yametoa  uhalisia wa jinsi gani ligi hiyo ilivyo na ushindani mkubwa kwani tumeshuudia viojana kutoka darajani (Chelsea ) wakilala goli moja kwa bila dhidi ya Crystal Palace.

Lakin kama hiyo haitoshi baada ya kupata matokeo mazuri katika mechi iliyopita dhidi ya wapinzani wao kutoka jiji moja la Manchester yani man  utd, leo Manchester city  walijikuta wakilazimishwa sare ya goli moja kwa moja dhidi ya vijana wa Arsena Wenger yani Arseanal  ambao wapo nafasi ya nne na pointi zao (64) katika msimamo wa ligi kwa hivi sasa, huku Manchester city wao wakishikilia nafasi ya tatu na pointi zao ( 67 ).

Chelsea yeye anaendelea kubaki na pointi zake zile zile (69) huku akiwa tayari ameshacheza michezo (32), tofauti na yule mabaye anashikilia nafasi ya pili huku akiwa na mchezo pungufu yani (31) na pointi (68) hao si wengine bali ni Liverpool ambao msimu huu naweza sema malengo yao ni kushiriki michuano ya mabingwa barani ulaya yani UEFA baada ya kutokuwepo zaidi ya misimu mitano sasa.

Lakini tukirudi darasani na kuzitumia vizuri kalamu na karatasi kwa msaada wa kikokotoa mahesabu ya calculator ndipo ninapokuja kugungua kuwa  Manuel Pelegrin ni mtu amabye anaweza kulinyakuwa taji hili la EPL kwa mara ya kwanza akiwa na kikosi cha Machester city kwani tayari anazo pointi (67) huku akiwa ameshuka dimbani mara 30 na inakuwa ni tofauti ya michezo miwili na kinara wa ligi hiyo kwa sasa yani Chelsea mwenye pointi (69).

Kwa mahesabu waweza bashiri hivyo lakini kiukweli bado ligi hii inazidi kuchanganya, na ukizingatia bingwa mtetezi nangali bado anasuasua katika nafasi ya saba akiwa na pointi zake (54) huku akiwa tayari na michezo (32).

 Huku nafasi ya juu yake inamilikiwa na Tottenham wakiwa na pointi (56) na michezo (31), na nafasi ya tano inamilikiwa na Everton akiwa na pointi (57) na michezo (30), kwa mana hiyo bado kuna upinzani wa kutosha na chochote kinaweza kutokea na kushuhudia aliye juu akashuka chini, na aliye chini akapanda juu.

1 comment: