Hakika hapa ndipo unapotumika ile kauli ya kusema kuwa asiye
fanya kazi na asile, ama kila mbuzi atakula kwa urefu wa kamba yake, hii nia baadhi ya misemo ambayo hupendwa
kutumiwa na wengi pindi panapokuwa na ushindani mkubwa wa kitu flani.
Nimeamua kutumia kauli hizi mbili au misemo hii miwili
ambayo ina mana moja nazani katika matumizi ya kila siku.
Huku Pep Guadiola akikamilisha mapema tu kazi ya maafisa wa
ligi kuu ya ujerumani na kuwapa nafasi
ya kupanga ratiba ya msimu ujao baada ya kuchukuwa ndoo ya ubingwa mapema tena
akiwa na mechi saba mkononi na pia akiweka rekodi ya kipekee zaidi na kikosi
cha bayern munich.
Lakini mambo yamekuwa tofauti sana kwa baadhi ya ligi kuu
barani ulaya, hususani kwa ligi kuu ya
wingereza maarufu kama ( EPL ), kwani hadi kufikia sasa bado hajajulikana na
atakaye tangazwa bigwa mwishoni mwa
msimu huu kati y Chelsea, Man cty, Liverpool, ama Arsenal.
Timu hizi zote bado zina nafasi ya kuchukuwa taji la ligi
kama kila mmoja atatumia vizuri makosa atakayo yafanya mwenzake kwa wakati huu
uliobakia kwenda kukamilisha mzunguko wa ligi hiyo, lakini ugumu unakuja
kutokana na matokeo ambayo yamekuwa yakifanya ligi hii ya EPL
kutumia ile misemo niliyo anzanayo mwanzo kabisa.
Baadhi ya matokeo ya leo katika ligi hiyo naweza seama
yametoa uhalisia wa jinsi gani ligi hiyo
ilivyo na ushindani mkubwa kwani tumeshuudia viojana kutoka darajani (Chelsea )
wakilala goli moja kwa bila dhidi ya Crystal Palace.
Lakin kama hiyo haitoshi baada ya kupata matokeo mazuri
katika mechi iliyopita dhidi ya wapinzani wao kutoka jiji moja la Manchester
yani man utd, leo Manchester city walijikuta wakilazimishwa sare ya goli moja
kwa moja dhidi ya vijana wa Arsena Wenger yani Arseanal ambao wapo nafasi ya nne na pointi zao (64)
katika msimamo wa ligi kwa hivi sasa, huku Manchester city wao wakishikilia
nafasi ya tatu na pointi zao ( 67 ).
Chelsea yeye anaendelea kubaki na pointi zake zile zile (69)
huku akiwa tayari ameshacheza michezo (32), tofauti na yule mabaye anashikilia
nafasi ya pili huku akiwa na mchezo pungufu yani (31) na pointi (68) hao si
wengine bali ni Liverpool ambao msimu huu naweza sema malengo yao ni kushiriki
michuano ya mabingwa barani ulaya yani UEFA baada ya kutokuwepo zaidi ya misimu
mitano sasa.
Lakini tukirudi darasani na kuzitumia vizuri kalamu na
karatasi kwa msaada wa kikokotoa mahesabu ya calculator ndipo ninapokuja
kugungua kuwa Manuel Pelegrin ni mtu
amabye anaweza kulinyakuwa taji hili la EPL kwa mara ya kwanza akiwa na kikosi
cha Machester city kwani tayari anazo pointi (67) huku akiwa ameshuka dimbani
mara 30 na inakuwa ni tofauti ya michezo miwili na kinara wa ligi hiyo kwa sasa
yani Chelsea mwenye pointi (69).
Kwa mahesabu waweza bashiri hivyo lakini kiukweli bado ligi
hii inazidi kuchanganya, na ukizingatia bingwa mtetezi nangali bado anasuasua
katika nafasi ya saba akiwa na pointi zake (54) huku akiwa tayari na michezo
(32).
Huku nafasi ya juu yake inamilikiwa na Tottenham wakiwa na pointi (56) na
michezo (31), na nafasi ya tano inamilikiwa na Everton akiwa na pointi (57) na
michezo (30), kwa mana hiyo bado kuna upinzani wa kutosha na chochote kinaweza
kutokea na kushuhudia aliye juu akashuka chini, na aliye chini akapanda juu.