Mambo ambayo
yanaweza kutokea na kuwa historia mpya na ya kipekee katika soka hususani
katika ligi ya mabingwa barani ulaya yani UEFA, kwa msimu huu ambao tumeweza
kushuhudia vilabu mbalimbali vikitoa upinzani wwa kutosha kwa vilabu kongwe
katika ligi hiyo.
Tukianza na
klabu ya Atletico de Madrid akiongozwa na Diego Simione ameweza kutoa upinzani
mkubwa sana msimu huu akianzia katika ligi kuu ya spain yani La Liga na hadi
sasa inaongoza ligi hiyo kwa tofauti ya pointi nne dhidi ya Barcelona.
Atletico imeingia
katika hatua ya nusu fainali kwa kuwasambaratisha vizuri tu vigogo wengine
kutoka katika ligi moja nao ambao ni fc Barcelona kwa jumla ya magoli 2 kwa 1
na hivyo kupelekea wao kuweza kuingia katika hatua hiyo ya nusu fainali na
kukutana na Chelsea.
Kama
watafanikikupita kupita katika hatua hii
na kuingia fainali na kufanikiwa kuchukua kombe hili namba mbili kwa umarufu
duniani basi watakuwa wameweka rekodi mpya katika klabu tangia kuanzishwa
yapata miaka 40 sasa kuchukuwa kombe hilo la UEFA kwa mara ya kwanza, Hiyo
itakuwa ni kwa upande wa wababe hawa wapya wa ligi ya spain.
Kwa upande
wa mabingwa wapya na wa kihistoria wa Ujerumani Bayern wao wameweza kuingia
kwenye hatua ya nusu fainali baada ya kuwachabanga vilivyo mashetani wekundu wa
jiji la manchester kwa jumla ya magoli 4 kwa 2 na kukata tiketi hiyo na sasa
watkutana na Real Madrid.
Klabu hii
inayongozwa na kocha aliyejizolea
makombea mbalimbali akiwa na Fc Barcelona Pep Guadiola kama itaweza kuchukuwa
kombe hili basi itakuwa ni timu ya kwanza katika historia ya michuano hii
kubeba kombe hili mara mbili mfululizo kwani wao ndo mabingwa watetezi hadi
hivi sasa.
Kwa upande
wa klabu ya Chelsea inayonolewa na kocha
mreno mwenye maneno mengi kama wasemavyo mashabiki wa soka dunia kwa ujumla
Jose Mourinho, kama itafanikiwa kuchukua kombe hili basi itakuwa ni historia
mpya kwa kocha huyo kuchukuwa kombe hili mra tatu akiwa na timu tatu tofauti na
katika nchi tatu tofauti duniani.
Nao Real
Madrid ambayo imeweza kuchukuwa kombe hili kwa mara 9 na kuwa klabu inayo
ongoza katika hisoria ya michuano hii, basi kama itaweza kubeba tena kombe hili
itakuwa ndiyo klabu ya kwanza katika historia kuweza kufikia nambari 10 au (
double digit number )
Je ni nani
ataweza kuibuka mshindi na kuweka historia mpya katika klabu yake kati yao?,
hili ni swali ambalo nazani tunaweza kulijibu kunako usiku wa tarehe 22 mwezi
huu kati nchi ya Spain ambapo ndipo mechi zote za hatua ya nusu fainali
zitaanzia.