Jinamizi la majeruhi limeendelea kuwandama mabingwa watetezi wa ligi kuu ya England Chelsea, baada ya safari hii wodi yao kumpokea captain John Terry.
Terry aliumia kwenye mchezo wake wa 699 akiwa na jezi ya Chelsea dhidi ya Newcastle United, huku wakiibuka na ushindi wa magoli 5-0.
Taarifa za ndani zinasema kuwa Terry ameshindwa kusafiri na timu jioni ya leo kwenda ufaransa katika pambano la michuano ya uefa champion league hatua ya mtoano dhidi ya PSG.
Lakini pia taarifa nzuri ni kuwa mchezaji aliye katika kiwango cha juu kwa sasa Oscar amerejea kikosi na kufanikiwa kusafiri na timu ..
Kwa upande mwingne Terry atalazimaka kusubiri kupona ili kukamilisha mchezo wake wa 700 akiwa na kikosi chake hiko kabla ya kuachana na miamba hyo ya London mwishoni mwa msimu huu
Source :skysports